Kuswali nyuma ya imamu msherekeaji kindakindaki wa maulidi

Imamu huyu ambaye anawaswalisha watu anatakiwa kupewa nasaha aachane na jambo hili. Kuswali nyuma yake ni sahihi, ikiwa hafanyi jengine zaidi ya maulidi, swalah nyuma yake ni sahihi. Kwa sababu maulidi ni Bid´ah na sio ukafiri. Lakini ikiwa katika maulidi hayo wanamuomba Mtume na wanamtaka msaada, basi hiyo ni kufuru kubwa. Ikiwa wanamuomba Mtume, wanamtaka msaada na wanamuwekea nadhiri basi hiyo ni kufuru kubwa. Ama kusherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanakusanya chakula, wanakusanyika kwa ajili ya chakula na wanasoma mashairi yasiyokuwa na shirki ni Bid´ah tu. Kuhusu mashairi yaliyo na shirki, kama mfano wa al-Burdah, wakikubali ile shirki inayopatikana ndani yake kwa mfano pale anaposema:

Ee kiumbe mbora! Sina mwengine zaidi yako wa kumkimbilia wakati wa majanga

Usiponitukuza siku ya Qiyaamah na ukanishika mkono, nimeangamia.

Katika ukarimu wako ni pamoja na dunia hii na mali zake

na miongoni mwa elimu zako ni pamoja na elimu ya Ubao na Kalamu.

 Mwenye kuyaamini haya ni kafiri.

Tunachokusudia ni kwamba waislamu wanatakiwa kutahadhari shirki na Bid´ah zote. Wanatakiwa washauriane kuziacha. Waelewe na kujifunza dini yao. Wanapaswa kuwauliza wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah juu ya Bid´ah hii. Tunamuomba Allaah awaongoze watu wote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdu-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/15333/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%AD%D8%AA%D9%81%D8%A7%D9%84-%D8%A8%D9%85%D9%88%D9%84%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%A8%D9%8A-%EF%B7%BA-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D8%AE%D9%84%D9%81-%D9%85%D9%86-%D9%8A%D8%AD%D8%AA%D9%81%D9%84-%D8%A8%D9%87
  • Imechapishwa: 16/11/2019