Kuswali nyuma ya imamu anayezusha baada ya swalah


Swali: Je, kuna kigezo cha Adhkaar? Tunaona namna ambavo kuna vikundi ambavyo khaswa wanatenga wakati maalum baada ya swalah ya Maghrib ambapo wanasoma Dhikr kwa sauti ya juu.

Jibu: Kigezo katika Adhkaar na ´ibaadah nyenginezo zote ni kwamba kitendo kiwepo katika Sunnah. Kile kilichomo katika Sunnah ni sahihi. Kile kisichokuweko katika Sunnah ni Bid´ah. Msingi katika ´ibaadah zote ni kujizuia mpaka kuthibiti dalili inayoonyesha kinyume na hivo. Hawa ambao wanakusanyika baada ya Maghrib na wanasoma Takbiyr na Tasbiyh kwa sauti ya juu na kwa sura ya pamoja kuna dalili ya kitu kama hichi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au Maswahabah? Hakuna. Muda wa kuwa ni kitu hakikupokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah waongofu basi sio Sunnah bali ni Bid´ah iliyokatazwa.

Swali: Baada ya swalah ya Maghrib wanaswali [swalah ya sunnah] kwa pamoja. Baada ya kumalizika kwa swalah wananyanyua sauti zao na khaswa imamu na kisha maamuma baada yake.

Jibu: Kuswali swalah ya sunnah kwa pamoja hakufai isipokuwa kwa kile kisichosapotiwa na Sunnah; swalah tano za faradhi, Tarawiyh katika Ramadhaan, swalah ya kupatwa kwa jua (ikiwa tutasema kuwa ni sunnah) na swalah ya kuomba kunyesha mvua. Kuhusu Rawaatib na swalah ya usiku ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah kuziswali kwa mkusanyiko. Hata hivyo hapana neno kufanya hivo katika baadhi ya nyakati. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivo na Ibn ´Abbaas, Ibn Mas´uud na Hudhayfah bin al-Yamaan.

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali na mkusanyiko huu khaswa kwa kuzingatia kwamba wametenga maalum wakati huu… ?

Ibn ´Uthaymiyn: Unakusudia kwamba wewe unaswalishwa…

Muulizaji: Ndio, naongozwa na imamu.

Jibu: Hapana vibaya kuswali pamoja nao. Bid´ah hii haimtii katika ukafiri. Hapana neno kuswali nyuma yake. Kwa sababu Bid´ah hii sio ya ukafiri. Lakini ukichelea kwamba kuswali kwako nyuma yake kunamtia yeye au wengine katika mtihani, katika hali hii usiswali nyuma yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (9 B)
  • Imechapishwa: 21/07/2021