Kuswali nyuma ya imamu anayefanya Qunuut Fajr

Swali: Kuna baadhi ya miji ya Kiislamu wapo maimamu wanakunuti katika swalah ya Fajr. Je, wafuatwe katika hilo?

Jibu: Ndio, wafuatwe. Lakini maoni sahihi ni kwamba asifanye Qunuut isipokuwa wakati wa majanga. Lakini ukiswali nyuma ya imamu na wewe kunuti na wala usitofautiani naye. Hapa mswaliji anatakiwa kuachana na maoni yake na badala yake afuate maoni ya imamu. Ukiswali nyuma ya ambaye anafanya Qunuut na wewe unaonelea kutofaa kukunuti, swali nyuma yake na wala usitofautiani naye. Kwa sababu baadhi ya wanachuoni wanaonelea kufaa kufanya hivo, kama mfano wa Shaafi´iyyah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 11/09/2018