Kuswali nyuma ya imamu anayeamini Allaah yuko kila mahali

Swali: Katika mji wangu watu wengi wanaamini kuwa Allaah yuko kila mahali na maimamu wa misikiti huku wako katika hali hiyo. Je, niswali peke yangu, niswali nao au niswali nao ijumaa tu?

Jibu: Ukijua kuwa imamu anaamini ´Aqiydah hii, usiswali nyuma yake. Ama ikiwa hujui, msingi kwa muislamu ni kuwa kheri na uadilifu. Hili linahusiana na pale ambapo hujui.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (78) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/taf_3_1_1433.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020