Kuswali ndani ya gari inapokhofiwa kushuka


Swali: Nilikuwa msafiri na nilikuwa pamoja na mke wangu na watoto. Ukaingia wakati wa swalah ya al-Fajr na njia ni yenye kutia khofu. Nikakhofia juu ya nafsi yangu na watoto wangu na hivyo sikuswali mpaka wakati ulipotoka. Je, kitendo changu hichi ni sahihi?

Jibu: Ikiwa kuteremka hakuaminiki kwa familia yako, mgeswali ndani ya gari swalah ya khofu. Mgeswali ndani ya gari na huku mko mnaenda. Swalah inaswaliwa kwa wakati wake kwa kiasi mtu atavyoweza:

فَإِنْ خِفْتُمْ فَرِجَالًا أَوْ رُكْبَانًا

“Mkikhofu hali mnakwenda au mmepanda kipando.” (02:239)

Mgeliswali ndani ya gari. Shutameni wakati wa Rukuu´ na Sujuud ilihali mmeikaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (49) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-5-13.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014