Kuswali na wudhuu´ ambao mtu hakunuia kuswali nao

Swali: Inajuzu kwa mtu kuswali na wudhuu´ aliyotawadha ambao hakunuia kwao swalah?

Jibu: Mtu akitawadha pasi na nia ya swalah, bali ametawadha kwa ajili ya kuondosha hadathi peke yake inafaa kwake kuswali swalah za faradhi na za sunnah anazotaka mpaka wudhuu´ utapomchenguka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/148)
  • Imechapishwa: 01/07/2017