Kuswali na nguo yenye damu nyingi

Swali: Nguo za vijana hupatwa na damu baada ya kutoka mawindoni na wanataka kwenda kuswali katika hali hiyo. Ni ipi hukumu ya kuswali ndani ya nguo hizi?

Jibu: Ni lazima kuziosha ikiwa damu ni nyingi. Kwa sababu damu ni najisi na khaswakhaswa ile damu yenye kuchirizika.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 21/06/2020