Kuswali na nguo yenye damu kidogo

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali kwenye nguo ilio na damu chache?

Jibu: Ikiwa anajua basi ni lazima kuiosha japokuwa ni ndogo. Ama akisahau au alikuwa hajui ambapo akaswali, basi swalah yake ni sahihi. Akikumbuka katikati ya swalah aivue akiweza kufanya hivo. Asipoweza na damu hiyo ikawa juu ya kanzu yake aivue. Asipoweza kabisa basi aikate swalah yake na aoshe damu hiyo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (08) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191309#219638
  • Imechapishwa: 11/01/2019