Swali: Ni ipi hukumu ya manii yaliyoingia kwenye nguo? Ni masafi au najisi?

Jibu: Maoni ni masafi kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Yakiingia nguoni na ukaswali nayo swalah ni sahihi. Lakini bora ayakwangure yakiwa ni makavumakavu na ayaoshe yakiwa na unyevuunyevu. Hili ndio bora zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa salam) alikuwa akiyaosha na ´Aaishah alikuwa akiyakwangura  kutoka katika nguo yake yakiwa ni makavumakavu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4074/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D8%A7-%D9%8A%D8%B5%D9%8A%D8%A8-%D8%A7%D9%84%D8%AB%D9%8A%D8%A7%D8%A8-%D9%85%D9%86-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%86%D9%8A
  • Imechapishwa: 19/05/2020