Kuswali na nguo ambazo mtu ameota ndani yake

Swali: Inajuzu kuswali ndani ya nguo ambazo mtu ameziotea ndani yake?

Jibu: Ndio, inajuzu kuswali ndani ya nguo alizootea ndani yake. Isipokuwa inatakiwa kuosha manii yakiwa ni unyevunyevu na ayaparueparue yakiwa ni makavu. Hapa ni pale ambapo amelala baada ya kujisafisha na maji au kujisafisha na mawe kunakofaa Kishari´ah. Ama ikiwa amelala pasi na kujisafisha kwa maji wala kujisafisha kwa mawe kunakofaa Kishari´ah, basi haifai kuswali na nguo ambayo imeingiwa ndani yake manii haya mpaka kwanza aioshe. Hayo ni kwa sababu manii yakikutana na sehemu ile ya najisi itachafuka. Ikichafuka na nguo ikapatwa basi italazimika kuiosha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (10) http://binothaimeen.net/content/6735
  • Imechapishwa: 14/11/2020