Kuswali na kikoi peke yake na kitovu kuonekana

Swali: Inajuzu kuswali na kikao kinachofunika baina ya kitovu na magoti? Ni ipi hukumu ikiwa kitovu kitaonekana?

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba hakuna neno mtu akiswali na kitovu. Lakini ikiwa kikoi chake ni kipana kiasi cha kwamba anaweza kukivaa kama kikoi na vilevile kufunika mabega yake basi hapo itakuwa ni wajibu kwake. Ama ikiwa hana zaidi ya kikoi, hakuna neno akaswali kwenye kikoi. Lakini akiwa na kitu anachoweza kwacho kufunika mabega basi afanye hivo. Kitovu kikibaki wazi avute kikoi chake. Kwa sababu viungo visivyotakiwa kuonekana ni kati ya kitovu na magoti. Kitovu hakiingii katika viungo visivyotakiwa kuonekana na vivyo hivyo magoti sio katika viungo visivyotakiwa kuonekana. Lakini akipandishe. Kwa sababu kuna khatari atapotikisika kikashuka zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1407
  • Imechapishwa: 12/12/2019