Kuswali na familia baada ya kuchelewa msikitini

Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye amepitwa na swalah ya mkusanyiko kwa sababu ya kulala au sababu nyingine? Je, awaombe familia yake waswali pamoja naye ili aweze kupata fadhilah za swalah ya mkusanyiko?

Jibu: Akiswali pamoja nao ni sawa. Mwanamke hapangi safu pambizoni mwa mwanaume. Bali anatakiwa kuwa nyuma yake. Haijalishi kitu hata kama ni mume wake au baba yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 19/07/2019