Kuswali msikitini mkusanyiko kabla ya Iqaamah bila idhini ya imamu

Swali: Kundi la watu waliingia msikitini kabla ya kukimiwa swalah ambapo wakaswali kabla ya Iqaamah. Ni ipi hukumu ya swalah yao?

Jibu: Haijuzu kwa mtu kuanzisha mkusanyiko kwenye msikiti ulio na imamu aliyepangwa isipokuwa kwa idhini ya imamu. Watu hawa wakisema kuwa ni wasafiri na kwamba hawawezi kusubiri mpaka atapokuja imamu na akawaswalisha. Basi tunawaambia kwamba mambo ni sahali; mkiwa ni wasafiri basi endeleeni na safari na swalini njiani. Ama kuswali ndani ya msikiti ulio na imamu rasmi kabla ya kufika imamu ni jambo lisilofaa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kufanya hivo na akasema:

“Asimwongoze mtu mwingine katika utawala wake.”

Mtawala wa msikiti ni yule imamu wake. Kwa hivyo ni wajibu kusubiri mpaka pindi imamu atapofika. Wakisema kuwa ni wasafiri na hawawezi kusubiri, basi tunawaambia kwamba ni wenye kupewa udhuru kuacha kuswali swalah ya mkusanyiko na hivyo safirini na swalini mahali kokote mtakotaka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1327
  • Imechapishwa: 07/11/2019