Kuswali kwenye msikiti uliojengwa na kafiri

Swali: Inafaa kuswali kwenye msikiti ambao kafiri ndiye kajitolea katika kuujenga?

Jibu: Bora misikiti ijengwe na waislamu. Lakini kafiri akisimamia zoezi la kujenga msikiti kutoka katika chumo la pesa ambayo ni halali, ndani yake haina haramu na pia kafiri huyo asiwe na kusudio baya juu ya waislamu, hakuna kikwazo kuswali ndani ya msikiti huu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=Lj91ZhPBbFA
  • Imechapishwa: 25/08/2020