Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swali kwa kusimama. Usipoweza, kwa kukaa. Usipoweza, kwa ubavu.”[1]

Ni vipi mtu anaswali kwa kulalia ubavu? Ni lazima iwe kwa ubavu wa kulia?

 Jibu: Ndio, bora ni kwa upande wa kulia. Asipoweza kufanya hivo, alale kwa upande wa kushoto. Hakuna neno. Hata hivyo uso unatakiwa kuuelekeza upande wa Ka´bah.

[1] al-Bukhaariy (1117).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (12) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-19-10-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 17/09/2017