Kuswali kwa kuelekea picha iliyotundikwa ukutani

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali mahala ambapo kumetundikwa picha kwenye ukuta?

Jibu: Haijuzu. Haisihi kuswali mahala ambapo kumetundikwa picha na mswalaji akawa ameielekea. Hili linafanana na ´ibaadah ya masanamu. Ama ikiwa haielekei, swalah ni sahihi na wakati huohuo madhambi bado yanabaki pale pale kwa kutundika picha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-2-10.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020