Kuswali kinyume na Qiblah ndani ya ndege

Swali: Nikiwa ndani ya ndege na ninataka kuswali Naafilah. Vipi nitaswali ilihali ndege haikuelekea Qiblah?

Jibu: Swali kule ulipoelekea. Isipokuwa ikiwa kama unaweza kuelekea Qiblah, hapo itakuwa ni wajibu kwako kuelekea. Ama ikiwa huwezi, swali upande wowote ambapo ndege itakuwa imeelekea, sawa ikiwa ni Swalah ya Naafilah au faradhi.

Swali: Kuna kauli (wanachuoni) wanasema kwamba atapiga Takbiyrat-ul-Ihraam ilihali ameelekea Qiblah kisha Swalah yake yote iliobaki ataelekea kule ambapo ndege itakuwa imeelekea.

Jibu: Ndio, ni kweli. Hili limepokelewa. Imepokelewa ya kwamba limefanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini kana kwamba (ni mapokezi ambayo) hayakuthibiti. Yametajwa pia kwenye Zaad al-Ma´aad.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-5-23.mp3
  • Imechapishwa: 09/11/2014