Kuswali Katika Chumba Kilicho Na Choo Cha Ndani

Swali: Katika majengo ya kisasa kumeenea kutengeneza choo ndani ya chumba cha kulalia. Je, inajuzu kuswali katika chumba hichi?

Jibu: Ndio. Kizuizi kiko wapi? Maadamu choo kimetengana na ukuta na baina yako wewe na choo kuna ukuta hakuna neno. Swali katika chumba hicho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (9) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340506.mp3
  • Imechapishwa: 15/04/2017