Kuswali kanisani au kwenye hekalu za Raafidhwah


Swali: Je, inafaa kuswali sehemu ambayo anaasiwa Allaah kama vile kuswali kanisani au hekalu za Raafidhwah?

Jibu: Haifai kuswaliaemo isipokuwa zikiondoshwa zile alama za shirki kama mfano wa al-Laat ambaye alikuwa katika msikiti wa Twaaif. Lilipoondoshwa Allaah akafanya sehemu hiyo msikiti unaoswaliwa ndani yake. Lakini mtu akilazimika kuswali ndani yake na sehemu hiyo ikawa safi hakuna neno. Katika hali hiyo aswali peke yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 08/04/2018