Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali kwenye nyesi mchi zinazopandwa kwenye mabustani na maeneo ya kupumzikia?

Jibu: Hapana neno kufanya hivo. Msingi ni kwamba ardhi yote ni safi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ardhi yote kwangu imefanywa kuwa ni safi na yenye kusafisha.”

Muda wa kuwa inamwagiliwa maji safi basi hapana shida yoyote.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 21/08/2021