Swali: Kuhusiana na suala la kuswali juu ya mkeka/msala msikitini. Ni jambo linalotambulika kwamba msikiti wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haukua na mkeka. Imepokelewa katika “as-Swahiyh” kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy kuhusu I´tikaaf ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo amesimulia kwamba alifanya I´tikaaf pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ndani yake imetajwa kwamba mwenye kufanya I´tikaaf basi arejee kwenye I´tikaaf yake na kwamba usiku huo aliona akisujudu juu ya maji na udongo. Isitoshe Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ameyataja mambo haya katika “al-Fataawaa al-Kubraa” (03/32-34).

Jibu: Kuswali juu ya mkeka/msala kwa njia ya kwamba mswaliji hawezi isipokuwa kuswali juu ya mkeka haikuwa mwenendo wa Salaf katika Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Bali walikuwa wakiswali juu ya ardhi. Hapakuwepo yeyote aliyetenga mkeka/msala kwa ajili ya kuswalia juu yake.

Imepokelewa kwamba ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy wakati alipofika al-Madiynah alitandaza mkeka/msala ambapo Maalik akaamrisha atiwe gerezani. Akaambiwa kwamba aliyefanya hivo ni ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy ambapo akajibu: “Je, hakujua kuwa kutandaza mkeka/msala msikitini kwetu ni Bid´ah?” Halafu baada ya hapo Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) akataja Hadiyth ya Abu Sa´iyd al-Khudriy ambayo imekwishatangulia na Hadiyth zengine zinazofahamisha juu ya hilo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alifta.net/fatawa/fatawaDetails.aspx?languagename=ar&BookID=3&View=Page&PageNo=6&PageID=11982
  • Imechapishwa: 02/02/2019