Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali juu ya mkeka/msala wenye marembo? Je, ni Bid´ah?

Jibu: Hapana, imechukizwa tu. Kwa sababu unamshawishi mtu na swalah yake. Bora ni yeye kuswali kwenye mkeka/msala wa kawaida usiokuwa na marembo ili usimshawishi yeye na swalah. Vilevile mtu anaweza kuswali juu ya ardhi safi. Ama kuhusu mikeka/misala iliyo na marembo inaweza kumshawishi mwenye kuswali. Kwa hiyo kuiacha ni bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/18970/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D8%A7%D9%84%D8%B3%D8%AC%D8%A7%D8%AF%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B2%D8%AE%D8%B1%D9%81%D8%A9
  • Imechapishwa: 02/02/2019