Kuswali ´Ishaa nyuma ya anayeswali Tarawiyh

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuswali faradhi nyuma ya ambaye anaswali swalah ya Sunnah kama mfano wa yule anayeswali ´ishaa nyuma ya anayeswali Tarawiyh?

Jibu: Hakuna neno kuswali ´ishaa nyuma ya anayeswali Tarawiyh. Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesimulia hilo. Akiwa ni msafiri na akajiunga na imamu mwanzoni mwa swalah atatoa Tasliym pamoja naye. Vinginevyo atakamilisha Rak´ah zilizobaki pale imamu atapotoa Tasliym.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/444)
  • Imechapishwa: 23/07/2017