Kuswali ´Ishaa nyuma ya anayeswali Tarawiyh II

Swali: Mwenye kufika kwa watu ambao wanaswali Tarawiyh na yeye ni msafiri au ambaye yuko na hukumu ya safari kama mkazi wa siku mbili mpaka tatu kisha anarudi ni sahihi kwake kuswali na imamu ambaye ni mkazi swalah ya ´Ishaa Rak´ah mbili kwa kufupisha ilihali imamu anaswali Tarawiyh?

Jibu: Ndio. Msafiri akiingia na imamu anayeswali Tarawiyh, aswali Rak´ah mbili kwa nia ya ´Ishaa na hakuna neno. Kwa kuwa hakwenda kinyume na Imamu. Hili ni tofauti na msafiri pindi anapoingia na Imamu mkazi anayeswali Rak´ah nne, katika hali hii ni lazima aswali Rak´ah nne hata kama atakuwa ameingia naye katika Rak´ah ya pili, ni lazima vilevile aswali Rak´ah mbili zingine zilizobaki baada ya Imamu kutoa Salaam.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mkanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 05
  • Imechapishwa: 23/09/2020