Swali: Je, ni kweli kwamba haifai kuswali swalah ya Fajr baada ya adhaana moja kwa moja bali mtu anatakiwa kusubiri muda kidogo?
Jibu: Adhaana inatangulizwa au inacheleweshwa? Swalah inatakiwa kuswaliwa pale ambapo Fajr inaaingia. Kuonekana kuingia kwa Fajr kuko wazi na si jambo la kujificha. Watazame mashariki. Endapo Fajr itakuwa imeshaingia basi waswali:
وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ
“Kulani na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe wa alfajiri kutokana na uzi mweusi.” (02:187)
Vivyo hivyo kuhusiana na swalah ya Fajr.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17412
- Imechapishwa: 10/12/2017