Kuswali dakika kadhaa kabla ya kuingia wakati wa swalah

Swali: Mtu akiswali takriban dakika 10 au chini ya hapo kabla ya kuingia wakati wa swalah pamoja na kuzingatia kwamba alikuwa hajui kuwa wakati umebadilika. Je, swalah yake inabatilika? Analazimika kuirudi baada ya kujua?

Jibu: Swalah yake aliyoiswali kabla ya kuingia wakati haimtoshelezi kutokamana na faradhi. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا

“Kwani hakika swalah kwa waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalum.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amebainisha nyakati hizi pale aliposema:

 “Wakati wa dhuhr ni pale jua linapotenguka na kikawa kivuli cha mtu kama mfano wa urefu wake… “

Kujengea juu ya haya yule ambaye ameswali swalah kabla ya kuingia wakati wake basi swalah yake haimtoshelezi kutokamana na faradhi. Lakini hata hivyo analipwa thawabu za swalah ya sunnah kwa swalah hiyo. Kutokana na hayo ni lazima kwake kuirudi swalah yake baada ya kuingia wakati.

[1] 04:103

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=b0GW4RDwN74
  • Imechapishwa: 25/04/2020