Kusuluhisha kati ya watu ni bora kuliko kuwahukumu


Hadiyth[1] inatupa dalili nyingine kwamba imesuniwa kusuluhisha hali za watu na kwamba ni jambo linalotakikana na inapaswa kwa wale wakuu kuwaombea baina ya watu wakati wa magomvi ili wasiendelee kugombana na kufanyiana vifundo na chuki. Kusuluhisha kati ya watu ni bora kuliko kuwahukumu. Hukumu inapelekea katika mizozo. Wakipatana kwa kuridhiana na ikaondoka ile chuki yote iliyomo vifuani mwao na mapenzi na mahaba yakafunguka inakuwa bora.

[1] Abu Shurayh ameeleza ya kwamba alikuwa akiitwa “Abul-Hakam”, baba wa wahakimu, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: “Allaah ndiye Hakimu na hukumu ni Yake.” Kisha Abu Shurayh akasema: “Hakika watu wangu wanapotofautiana katika kitu basi hunijia na nikahukumu baina yao na matokeo yake pande zote mbili huridhika.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ni uzuri ulioje wa jambo hilo! Kwani wewe huna mtoto?” Nikasema: “Shurayh, Muslim na ´Abdullaah.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ni nani mkubwa wao?” Nikasema: “Shurayh.” Ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Basi wewe ni Abu Shurayh.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 142-143
  • Imechapishwa: 15/11/2018