Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka ncha ya Shimaagh chini wakati wa swalah na mtu akasujudu juu yake ili mtu ajiepushe na vumbi na harufu mbaya?

Jibu: Ikiwa kuna haja ya mtu kusujudu juu ya Shimaagh, Ghutrah na Mishlah basi hakuna neno. Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Tulikuwa tukiswali pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati wa joto kali. Wakati mmoja wetu anaposhindwa kuweka paji lake la uso juu ya ardhi anaitandaza nguo yake na anasujudu juu yake.”

Kwa mfano ardhi ikiwa ni yenye joto kali, kuna miba au fimbo ambapo mtu hawezi kukakinisha paji lake la uso, basi hakuna neno akaweka ncha ya Ghutrah, Shimaagh na Mishlah na akasujudu juu yake. Lakini pasi na haja imechukizwa. Ama akisujudu juu ya kitu kilichojitenga pia hakuna neno. Kwa mfano mtu ana leso na alipotaka kusujudu juu ya ardhi akaweka leso yake, hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (49) http://binothaimeen.net/content/1128
  • Imechapishwa: 02/05/2019