Kusoma Suurah nyingine baada ya al-Faatihah imamu akirefusha

Swali: Katika swalah zenye Rak´ah nne pindi imamu anaporefusha katika Rak´ah ya pili na ya tatu baada ya mimi kumaliza kusoma al-Faatihah – je, nisome Suurah baada yake au ni lazima kunyamaza mpaka pale ataporukuu?

Jibu: Hapana, bora ni wewe kusoma Suurah nyingine baada yake. Kwa sababu imekuja katika Hadiyth ya Abu Sa´iyd yanayofahamisha kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaweza kuzidisha juu ya al-Faatihah katika zile Rak´ah mbili za mwisho. Jengine ni kwa sababu swalah haina unyamazo. Isipokuwa tu pale imamu anaposoma na imamu anasoma kimyakimya. Kujengea juu ya haya tunasema kuwa soma Suurah nyingine baada ya al-Faatihah.

Huenda akauliza mtu: “Je, nyinyi si mnaona kuwa haifai kuikariri al-Faatihah?”[1] Jibu ni hapana. Kwa sababu kufanya hivo hakukupokelewa. Ama kusoma Suurah nyingine baada ya al-Faatihah katika zile Rak´ah mbili za mwisho ni jambo limepokelewa.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/al-faatihah-haikaririwi/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (71) http://binothaimeen.net/content/1638
  • Imechapishwa: 29/03/2020