Kusoma Qur-aan ndani ya nyumba kuliko mbwa


Swali: Ni ipi hukumu ya kusoma Qur-aan ndani ya nyumba ambayo kuna mbwa?

Jibu: Hakuna neno kufanya hivo. Ni lazima mbwa atolewe nje na kutombakiza nyumbani. Isipokuwa ikiwa ni kutokana na sababu tatu:

1 – Mbwa wa mawindo.

2 – Mbwa kwa ajili ya kilimo.

3 – Mbwa ajili ya kukuelekeza njia.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye anayemiliki mbwa – isipokuwa mbwa wa uwindaji, kuelekeza njia au kilimo – basi kila siku inapungua kutoka katika ujira wake Qiraatw mbili.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (08/362)
  • Imechapishwa: 25/06/2021