Swali: Je, inajuzu kusoma Qur-aan sokoni katika wakati ambapo ninakuwa sina kazi?

Jibu: Hakuna ubaya kusoma Qur-aan katika duka lako au mahali pa kazi kwako, ukiwa na uwezo wa hilo utasoma utachoweza katika Kitabu cha Allaah, au utamdhukuru Allaah au utamswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Unapokuwa huna kazi, jishughulishe na kumdhukuru Allaah (´Azza wa Jalla); kwa kusoma Qur-aan, kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au kwa kusoma vitabu vyenye faida. Mambo yote haya ni mazuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 24/03/2018