Kusoma Qur-aan kabla ya swalah ya ´Iyd


Swali: Siku ya ´Iyd na kabla ya imamu kuingi sehemu ya kuswalia ´Iyd kuna baadhi ya watu wanajishughulisha na Takbiyr na wengine wanajishughulisha na kusoma Qur-aan. Baadhi ya wale ambao wako pale wakawakemea wale wanaosoma Qur-aan na wakasema bora zaidi ni wao kuleta Takbiyr na mwache kusoma Qur-aan. Ni wepi kati a hao wawili walio katika usawa?

Jibu: Usawa ni kuleta Takbiyr. Lakini mwenye kusoma Qur-aan hatakiwi kukemewa. Kwa sababu Qur-aan ni Dhikr bali ni miongoni mwa Adhkaar njema kabisa. Lakini pale ilipokuwa Dhikr ndio jambo maalum lililotengwa katika wakati huu na Qur-aan inaweza kusomwa wakati wowote, ikawa kuhifadhi Takbiyr ndio bora zaidi. Lakini hata hivyo haitakwi kuwakaripia wale wengine.

Kwa ajili hii ndio maana Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika hajj ya kuaga, walikuwepo ambao wanaleta Talbiyah na walikuwepo wengine wanaoleta Takbiyr. Hakukuwepo yeyote anayemkemea mwengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/925
  • Imechapishwa: 17/11/2018