Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Du´aa hairudishwi nyuma kati ya adhaana na iqaamah.”

Je, bora kwa mtu akiswali Raatibah msikitini anyanyue mikono yake kuomba du´aa mpaka wakati wa kukimiwa swalah au asome Qur-aan?

Jibu: Bora ni yeye kusoma Qur-aan. Kwa sababu usomaji wa Qur-aan ni du´aa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (106) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatoul%20lahfan-%2027-03-1441.mp3
  • Imechapishwa: 17/09/2020