Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kusoma katika masomo mchanganyiko ili baadaye alinganie katika Uislamu safi?

Jibu: Hapana, hapana… Swali hili linafanana na maswali mengine ambayo yanaingia chini ya kanuni ya Kiislamu ´lengo linasahilisha njia`. Mwanamke huyu anataka kusoma katika chuo kikuu ambapo wanamme na wanawake wamechanganyika. Kwa nini? Kwa sababu alinganie katika Uislamu. Anataka kusoma na baadaye alinganie katika Uislamu. Tunarudi tena kulekule; yeye anaichoma nafsi yake kwa ajili ya kuwanufaisha wengine. Atafanya makosa yasiyopewa udhuru. Kwa sababu yale yanayofunzwa katika vyuo vikuu vya hii leo sio mambo ambayo ni lazima kwa waislamu wote kuyajua. Kubwa liwezalo kusemwa ni mambo ambayo inatosha kwa baadhi ya waislamu kuyajua; wakiyajua baadhi ya waislamu basi wengine hawalazimiki kufanya hivo. Licha ya kuwa masomo ya leo madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake. Ni vipi basi hayo yatafanywa kuwa ni njia ya kulingania katika Uislamu?

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (31) Dakika: 38.35
  • Imechapishwa: 27/12/2020