Kusoma kwa sauti katika swalah za kusoma kimyakimya na kinyume chake

Swali: Je, kudhihirisha kisomo katika swalah za kusoma kwa sauti imependekezwa tu au ni wajibu? Je, imethibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba alisoma kimyakimya katika swalah za kusoma kwa sauti?

Jibu: Linalotambulika kwa wanachuoni ni kwamba kusoma kwa sauti na kusoma kimyakimya imependekezwa. Sikumbuki kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisoma kwa siri katika swalah za kusoma kwa sauti.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (01) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=190884#219018
  • Imechapishwa: 23/01/2018