Kusoma kimyakimya katika swalah za kusoma kwa sauti

Swali: Ni ipi hukumu ya kuacha kusoma kwa sauti katika zile swalah za kusoma kwa sauti?

Jibu: Kusoma kwa sauti na kusoma kimyakimya ni katika mambo yaliyopendekezwa kwa wanachuoni. Kwa hiyo kusoma kwa sauti na kusoma kimyakimya ni katika mambo ya Sunnah. Lakini kwa hali yoyote haitakikani kwa mtu kukusudia kuacha kusoma kwa sauti katika zile swalah za kusoma kwa sauti.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/88/%D8%AA%D8%B1%D9%83-%D8%A7%D9%84%D8%AC%D9%87%D8%B1-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%AC%D9%87%D8%B1%D9%8A%D8%A9
  • Imechapishwa: 05/01/2020