Kusoma Khutbat-ul-Haajah sehemu ya pili ya Khutbah peke yake

Swali: Nimemsikia mwanafunzi mmoja anasema kuwa anayetoa Khutbah ya Ijumaa kwa Khutbat-ul-Haajah tu basi Khutbah hii inatosheleza. Je, hili ni sahihi?

Jibu: Hapana, si sahihi. Khutbah ina nguzo zake. Khutbat-ul-Haajah ina himdi, sifa za Allaah, Shahaadah mbili na kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tu. Ndani yake hakuna mambo mengine ya Khutbah. Isitoshe haikuthibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anasoma Khutbat-ul-Haajah tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-11-09.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014