Kusoma du´aa kwa sauti ya juu


Swali: Baadhi ya watu wanasoma du´aa kwa sauti ya juu ambapo wanawashawishi walioko pambizoni mwao. Ni ipi hukumu ya kitendo chao hichi?

Jibu: Sunnah ni kusoma du´aa kimyakimya ndani ya swalah na kweginepo. Amesema (Subhaanah):

ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً

“Muombeni Mola wenu kwa unyenyekevu na kwa siri.”[1]

Jengine ni kwa sababu kufanya hivo ndio ukamilifu zaidi katika kumtakasia nia Allaah na kuukusanya moyo katika du´aa. Isitoshe kufanya hivo kunapelekea kutowashawishi waswaliji na wasomaji walioko kando nawe.

Lakini ikiwa du´aa ni ile ambayo kunaitikiwa “Aamiyn” kama mfano wa du´aa ya Qunuut na du´aa ya kuomba mvua, basi imamu anatakiwa kuisoma kwa sauti ya juu ili wasikilizaji waweze kuitikia “Aamiyn”.

[1] 07:55

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/397)
  • Imechapishwa: 28/07/2021