Kusoma du´aa kutoka kwenye karatasi ndani ya Tarawiyh

Swali: Mimi nimehifadhi du´aa chache. Je, inajuzu kwangu kuandika baadhi ya du´aa na kuzisoma nje ya swalah au katikati ya swalah?

Jibu: Hakuna kizuizi kwa mtu kusoma du´aa kutoka kwenye karatasi ikiwa hakuhifadhi ambapo akaziandika kwenye karatasi na kuzisoma katika nyakati ambazo anawajibika kuomba ndani yake. Mfano wa nyakati hizo ni mwisho wa usiku au katikati ya usiku. Lakini iwapo itakuwa ni sahali kwake kuzihifadhi moyoni na kwa unyenyekevu basi hilo litakuwa ni kamilifu zaidi. Ama kuzisoma ndani ya swalah bora ni kuzisoma kiyomoni ijapokuwa zitakuwa ni fupi. Ikiwa utazisoma kutoka kwenye karatasi kama kwa mfano katika Tashahhud au kati ya sijda mbil hakuna neno. Lakini yule mwombaji kuhifadhi du´aa anakuwa karibu zaidi na unyenyekevu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/31)
  • Imechapishwa: 21/05/2018