Kusoma dini ni bora zaidi kwako kuliko kingereza


Swali: Mimi ni msichana ambaye nimetakharuji katika chuo kikuu na nimesomea lugha ya kingereza. Unaonaje kuna ubaya nikiendelea na masomo ya juu?

Jibu: Mimi naona lau angelisomea elimu za Kishari´ah basi ingelikuwa bora zaidi kwake. Kwa sababu mimi nachelea kama amesomea lugha ya kingereza akachukua vitabu vya kingereza akapokea kutoka kwa makafiri na hatimaye akapotea kwavyo. Kama hivi sasa anaweza kuyafanya masomo yake yakawa ya Shari´ah katika chuo kikuu cha al-Imaam au katika vyuo vikuu vyengine, basi hili ni bora zaidi kwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (56) http://binothaimeen.net/content/1281
  • Imechapishwa: 09/10/2019