Swali: Je, kusoma Suurah “al-Kahf” siku ya alkhamisi baada ya Maghrib kunatosheleza kuisoma siku ya ijumaa?

Jibu: Kuna Hadiyth zilizopokelewa zinazofahamisha kuisoma usiku wa kuamkia ijumaa na kuisoma siku ya ijumaa. Kwa hivyo ni sawa kuisoma usiku wa kuamkia ijumaa baada ya Maghrib. Usiku wa kuamkia ijumaa unaanza baada ya jua kuzama. Siku ya ijumaa inaanza baada ya jua kuchomoza. Kwa hivyo imewekwa katika Shari´ah kuisoma Usiku wa kuamkia ijumaa na kuisoma pia siku ya ijumaa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa/AudioDir2/67880.mp3
  • Imechapishwa: 08/08/2017