Kusimamisha kucheza mpira na kuswali inapofika wakati wa swalah


Swali: Ninacheza mpira na baadhi ya marafiki zangu. Inapofika wakati wa swalah ya Maghrib huwaita tukaswali lakini wanakataa kwa hoja ya kwamba wananuka vibaya na hawana wudhuu´ na hoja nyinginezo. Je, aendelee nao au afanye nini?

Jibu: Ni wajibu pale wanaposikia adhaana waswali pamoja na waislamu, hili ni mamoja kwa wacheza mpira na wengine. Wanatakiwa kuswali pamoja na waislamu wenzao. Wasiache kwenda msikitini ikiwa kama wako karibu nao. Ikiwa msikiti uko mbali na wao waswali mahala walipo katika wakati wa swalah pamoja na waislamu wenzao. Waislamu wataposwali na wao waswali mahala pao. Wasijishughulishe na kucheza mpira na kuacha swalah na kuichelewesha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: at-Tahdhiyr min Du´aat-is-Suu'
  • Imechapishwa: 05/09/2020