Kusimama sehemu ya swalah na kuketi sehemu yake nyingine

Swali: Mwanamke ameleta Takbiyrat-ul-Ihraam, akaenda Rukuu´ na kuswali ile Rak´ah ya kwanza. Halafu hakuweza kusimama katika ile Raka´h ya pili. Kuanzia hapo akakamilisha swalah yake hali ya kukaa kwa sababu ni mgonjwa. Je, swalah yake katika hali hii ni sahihi?

Jibu: Ndio, swalah yake ni sahihi. Asimame pale atapoweza kusimama na akae akishindwa kusimama. Hayo yanaweza kutendeka katika swalah moja. Hakuna neno:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

“Mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (67) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah22-05-1438h.mp3
  • Imechapishwa: 18/10/2017