Swali: Yule ambaye anasikiliza mikanda ya Ahl-ul-Bid´ah au anasoma vitabu vyao kwa malengo ya kujua yale waliyomo. Je, mtu kama huyu anaingia katika wale wanaokaa na Ahl-ul-Bid´ah?

Jibu: Ni kama kukaa nao, au baya zaidi kuliko kukaa nao. Lakini ikiwa ni mjuzi na ni mtu mwenye elimu, akasikiliza na kuvisoma ili avipige Radd na kutahadharisha, hakuna ubaya kufanya hivyo. Ama ikiwa hana elimu wala Baswiyrah, anataka kusoma na kusikiliza, hili halijuzu. Kwa kuwa anaingia katika tuliowataja. Na hana kitu kinachomlinda navyo. Haijuzu kwake kusikiliza hali ya hana kinachomlinda na sumu na labaa ziliomo ndani yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=Kp4E83KiE30
  • Imechapishwa: 20/03/2018