Kusikiliza si kama mwenye kusoma


Swali: Nikisikiliza Qur-aan nazingatiwa ni kana kwamba nimeisoma?

Jibu: Hapana. Unazingatiwa kuwa umesikiliza na hukusoma. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ

“Inaposomwa Qur-aan basi isikilizeni na nyamazeni kimya ili mpate kurehemewa.” (07:204)

Kusikiliza kunakuwa kwa masikio na kusoma kunakuwa kwa mdomo. Kusoma ni bora kuliko kusikiliza. Kwa sababu ukisoma kila herufi moja ni jema moja na jema moja linalipwa kumi mfano wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 45
  • Imechapishwa: 19/06/2021