Swali 14: Ni ipi hukumu ya kushutama ambako kumefanana na Rukuu´ katika baadhi ya michezo kukiwemo karate? Kabla ya mechi kuanza wachezaji wanasimama hawa mbele ya hawa kisha wanainama kwa njia ya kusalimiana.

Jibu: Haijuzu kufanya hivo. Hii ni dhambi kubwa. Anajikurubisha kwake kwa taadhima kama hii kubwa. Hii ni shirki kubwa. Mtu kama huyo anatakiwa kufunzwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 33
  • Imechapishwa: 28/09/2018