Kushuka kwa Allaah usiku wa nusu ya Sha´baan kupitia upokezi wa Mu´aadh bin Jabal

77 – Abu Bakr ´Abdullaah bin Sulaymaan bin al-Ash´ath ametuhadithia: Hisham bin Khaalid ametuhadithia: Abu Khulayd ´Utbah bin Hammaad al-Qaariy ametuhadithia, kutoka kwa al-Awzaa´iy, kutoka kwa Mak-huul pamoja Ibn Thawbân, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Mak-huul, kutoka kwa Maalik bin Yukhaamir as-Saksakiy, kutoka kwa Mu´aadh bin Jabal, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Usiku wa nusu Sha´baan Allaah (´Azza wa Jall) huwatazama waja Wake na akawasamehe viumbe Wake wote isipokuwa mshirikina au ambaye moyoni mwake mna chuki.”[1]

[1] as-Sunnah (512) ya Ibn Abiy ´Aaswim. Shaykh al-Albaaniy amesema:

“Hadiyth ni Swahiyh na wapokezi wake ni waaminifu. Hata hivyo cheni ya wapokezi wake ni yenye kukatika kati ya Mak-huul na Maalik bin Yukhaamir. La sivyo ingelikuwa nzuri. Lakini Hadiyth ni Swahiyh kutokana na mapokezi mengine yanayoitilia nguvu. Hadiyth imekaguliwa katika “as-Swahiyhah”(1144).”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 166
  • Imechapishwa: 02/05/2020
  • taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy