Kushuka kwa Allaah usiku wa nusu ya Sha´baan kupitia upokezi wa Kathiyr bin Murrah al-Hadhwramiy 06

Kuhusu upokezi wa Burd bin Sinaan kutoka kwa Mak-huu, amesimulia:

88 – Abu Sahl bin Ziyaad ametuhadithia: al-´Umariy ametuhadithia: Nilimsikia ´Ammaar bin Abiy Shaybah akisema: Jariyr ametuhadithia: Kutokana na ninavojua ameipokea kutoka kwa Burd na Abul-´Alaa’ ash-Shaamiy, kutoka kwa Mak-huul, kutoka kwa Ka´b ambaye amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) hutazama viumbe Wake katika kila usiku wa nusu Sha´baan ambapo akawasamehe wote isipokuwa mshirikina au mwenye chuki.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 168
  • Imechapishwa: 09/05/2020