Kushuka kwa Allaah usiku wa nusu ya Sha´baan kupitia upokezi wa Kathiyr bin Murrah al-Hadhwramiy 05

Kuhusu upokezi wa Hishaam bin al-Ghaar kutoka kwa Mak-huul, ameitaja ´Abdullaah bin Sulaymaan kutoka kwa al-Ash´ath pasi na kuisikia kutoka kwake. Amesema:

86 – ´Abdullaah bin al-Isba´ al-Ba´lba´kiy ametuhadithia: al-Waliyd bin Muslim ametuhadithia: kutoka kwa Hishaam bin al-Ghaar, kutoka kwa Mak-huul, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Hadiyth mfano wa hii lakini hata hivyo yenyewe ni refu zaidi.

Ama kuhusu upokezi wa Ibn Abiy Hakiym kutoka kwa Mak-huul, ameeleza:

87 – Ahmad bin Muhammad bin Ziyaad ametuhadithia: al-Hasan bin ´Aliy bin Shabiyb ametuhadithia: Nilimsikia ´Amr bin ´Uthmaan akisema: Baqiyyah ametuhadithia: ´Utbah bin Abiy Hakiym ametuhadithia: Mak-huul amenihadithia: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) hutazama katika kila usiku wa nusu Sha´baan ambapo akamsamehe kila mja isipokuwa mshirikina au mwenye chuki.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 167-168
  • Imechapishwa: 09/05/2020