78- Abu Ja´far Muhammad bin Sulaymaan bin Muhammad an-Nu´maaniy ametuhadithia: ´Abdullaah bin ´Abdis-Swamad bin Abiy Khidaa ametuhadithia: ´Iysaa bin Yuunus ametuhadithia, kutoka kwa al-Ahwas bin Hakiym, kutoka kwa Habiyb bin Suhayb, kutoka kwa Abu Tha´labah al-Khushaniy ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) huwatazama waja Wake katika kila usiku wa nusu Sha´baan ambapo akawasamehe waumini, akawapa muhula makafiri na akawaacha wenye chuki na chuki zao mpaka waachane nazo.”[1]

[1] as-Sunnah (511) ya Ibn Abiy ´Aaswim. Shaykh al-Albaaniy amesema:

“Hadiyth ni Swahiyh na wapokezi wake ni waaminifu isipokuwa al-Ahwas bin Hakiym ambaye hifadhi yake ni nyonge, kama ilivyotajwa katika “at-Taqriyb”. Inaweza kutumiwa kwa lengo la shawahidi ambapo inatiliwa nguvu na njia zinazokuja mbele na mapokezi yaliyotangulia na mengine yatayotajwa.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 159-160
  • Imechapishwa: 04/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy